Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Esther Mahawe amewafaka wanawake wazalishaji na waandaaji wa kahawa katika wilaya hiyo kuzingatia mafunzo ili kukabiliana na changamoto katika mnyororo wa thamani wa kahawa wakiwa kama timu.
Mkuu huyo wa Wilaya ametoa rai hiyo leo Jumapili Julai 23, 2023 wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha wanawake wazalishaji na waandaaji wa kahawa kwa Wilaya ya Mbozi kilichofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Vwawa Day.
Kikao hicho kilikuwa na lengo la kuwaunganisha wanawake wote waliopo katika uzalishaji na uandaaji wa kahawa na shirika la International Women Coffee Alliance (IWCA) ili waweze kujengewa uwezo, kutafuta masoko na kupata bei rafiki ya kahawa.
Katika kikao hicho DC Mahawe amesema kuwa wilaya hiyo ina vyama vya msingi vya mazao 113 ambavyo vinakusanya kahawa na mazao mengine mchanganyiko.
"Asilimia 90 ya kahawa sawa na kiasi cha kilo 8,112,956 za kahawa inayozalishwa Mbozi ni kutoka kwa wakulima wadogo na asilimia 70 ya nguvu kazi na waandaji wa kahawa ni wanawake" amesema na kuongeza;
"Kwa miongo kadhaa kahawa imekuwa zao la kiume. Kwa kuona changamoto hii, fursa zilizopo tumeona ni muhimu wanawake wakaifahamu IWCA ili waweze nufaika na fursa zilizopo zikiwemo za uuzaji wa kahawa"
International Women Coffee Alliance (IWCA) ni shirika lisilo la kiserikali lenye madhumuni ya kuwasaidia wanawake wazalishaji na waandaaji wa kahawa katika kufikia bei nzuri ya kahawa na kuwajengea uwe
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa