• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Mbozi District Council
Mbozi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango , Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Idara ya Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mipango Miji na Maliasili
    • Vitengo
      • Wakaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Mipango na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
      • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
    • Majarida Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio

DC MAHAWE AWATAKA WANANCHI KUPELEKA WATOTO KUPATA CHANJO YA POLIO MBOZI

Kurushwa hewani: September 12th, 2023

Mkuu wa Wilaya ya Mbozi mkoni Songwe, Esther Mahawe amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa wahudumu wa afya watakaopita katika maeneo yao kutoa chanjo ya ugonjwa wa Polio huku akiwashauri wananchi  wa Wilaya hiyo kupuuza baadhi ya watu wanaopotosha juu ya chanjo hiyo.

 

Mkuu huyo wa Wilaya ametoa rai hiyo leo Jumanne Septemba 12, 2023 baada ya unzinduzi wa chanjo ya Polio awamu ya pili katika Wilaya hiyo ambapo amesema wapo baadhi ya watu wanapotosha juu ya mambo yanayofanywa na Serikali hivyo wananchi wachukue tahadhari.

Amesema kuwa ugonjwa huo ambao hauna tiba ni hatari kwa watoto chini ya miaka nane hivyo wazazi na walezi wahakikishe watoto wao wanapata chanjo hiyo itakayowazuia na maambukizi ya ugonjwa huo kwa kuwa chanjo hiyo haina madhara.

“Niendelee kuomba wananchi wote wanapotembelewa majumbani na wataalamu wetu wa afya watoe ushirikiano ili waweze kupatiwa elimu hii” ameeleza

“Leo katika uzinduzi tumekuwa na wakuu wa idara za shule za msingi na viongozi wa dini, nimeomba sana watu hao watusaidie kwasababu wanakutana na makundi mengi ya watu” amesema

 

Amesema kuwa wamekubaliana na viongozi wa dini wawaruhusu wataalamu wa afya kutoa elimu kwenye nyumba za ibada ikiwemo makanisani na misikitini ili elimu hiyo kuweza kuwafikia walio wengi.

DC Mahawe ameeleza kuwa athari ya ugonjwa huo ni pamoja na kusababisha ulemavu wa kudumu pale unapompata mtu.

“Ugonjwa huyu unasababisha ulemavu wa kudumu tangu kuambukizwa hadi kifo hivyo ni vizuri tukachukua tahadhari kabla ya hatari. Niwaombe wananchi wa wilaya ya Mbozi wote tuepuke wale watu watakaokuja na upotoshaji wakati watu wa afya wakiwa wanapita kutoa elimu hizi una watu wanapenda kupotosha jamii mambo mazuri yanayofanywa na Serikali ” ameeleza

 

Amesema kuwa wananchi wanapaswa kuchukua tahadhari kwa kuwa tayari mgonjwa mmoja amegundulika kuwa na polio katika mkoa wa Rukwa.

“Rukwa ni mkoa jirani na sisi kwa hiyo tuchukue tahadhari na sisi hatuko salama na sisi hatuishi kisiwani ni Imani yangu wananchi wa Wilaya ya Mbozi watachukua tahadhari” amesisitiza

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA March 09, 2025
  • RASIMU PENDEKEZWA YA SHERIA NDOGO ZA MWAKA 2025. March 09, 2025
  • Ona vyote

Habari Mpya

  • DC MBEGA AWATAKA VIONGOZI WA KATA KUSHIRIKIANA KATIKA UTENDAJI

    March 21, 2025
  • DC MBEGA AGAWA SARE ZA SHULE KWA WANAFUNZI 120 WANAOTOKA MAZINGIRA MAGUMU ISANGU

    March 21, 2025
  • DC MBEGA AFANYA ZIARA KUSIKILIZA NA KUTATUA KERO ZA WANANCHI, ASISITIZA USHIRIKIANO KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    March 19, 2025
  • DC MBEGA ASISITIZA UIMARISHAJI NA USIMAMIZI MZURI WA AMCOS MBOZI

    March 18, 2025
  • Ona vyote

Video

VIJANA MSITUMIE MIKOPO YA 10% KUBET MBOZI
video zaidi

Kurasa za Karibu

  • You Tube
  • Katiba

Tovuti Muhimu

  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Ikulu
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

Watembeleaji wa kimataifa

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

writingMasterThesis

Eneo la ramani

Wasiliana nasi

    Mbozi

    Anuani: 3

    Simu: 025-2580272

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa