Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Mhe. Esther Mahawe amewaasa wananchi wa Mbozi kuendelea kujikinga na maambikizi ya virusi vya UKIMWI kutokana na Wilaya hiyo kuwa na takwimu za juu kuliko viwango vile vya kitaifa.
Rai hiyo ameitoa leo Jumatano Novemba 29, 2023 katika Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani kiwilaya ambayo yamefanyika katika viwanja vya Wantanda Kata ya Isansa.
Katika hotuba yake Mkuu wa Wilaya huyo amesema kuwa Mbozi ni miongoni mwa Wilaya za mkoa wa Songwe zinazokabiliwa na kuwapo kwa changamoto ya kuwepo kwa tatizo la VVU/UKIMWI.
"Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI ni jukumu la Kila mwanajamii mahali alipo ambapo sera ya taifa inalenga kufikia 2030 Tanzania isiwe na maambikizi mapya ya VVU/UKIMWI" amesema na kuongeza;
"Serikali inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hasan imedhamiria kupunguza kiwango cha maambukizi ya ugonjwa huo kwa kutoa elimu juu ya njia za kujikinga na ugonjwa huo" ameeleza
"Kutokana na kukithiri kwa maambikizi ya ugonjwa huo wananchi tunatakiwa kuepuka ubaguzi na unyanyapaa kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI, ukatili wa kijinsia, ngono isiyo salama, unywaji pombe uliokithiri, kushiriki ngono katika umri mdogo, ubakaji na ulawiti"
Kauli mbiu ya maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani mwaka 2023 ni "Jamii iongoze kutokomeza UKIMWI"
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa