Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Mhe Esther Mahawe awataka waheshimiwa madiwani na wataalam ngazi ya kata kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yao.
Pia, Mhe. Mahawe amewasisitiza madiwani na wataalam katika Halmashauri kutekeleza maagizo ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Daniel Chongolo kujipanga katika utekelezaji wa maagizo ya Kamati za Bunge na hoja za mkaguzi wa ndani.
Mkuu huyo wa Wilaya amesema hayo leo Jumatano Mei 15, 2024 wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi.
"Ni jukumu letu kuhakikisha tunazuia hoja zisizokuwa na msingi na pia kuhakikisha majibu yanapatikana pindi zinapojitokeza. Vituo vyote vya afya kuhakikisha vinafungwa mfumo wa GOTHOMMIs ili kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato" amesema
"Kuhusiana na maelekezo ya kutanua vyumba vya biashara katika eneo la stendi ya Mlowo maelekezo ya mkuu wa mkoa amesisitiza wataalamu watakao simamia ugawaji wawe wenye weledi na tuhakikishe tunatekelezwa kwa wakati"
Amesema kuwa utekelezaji wa agizo hilo la ukarabati wa miundombinu ya stendi ya Mlowo utafanyika kwa wakati.
"Lingine ni mapato nawapongezeni sana kwa hatua mliofikia umoja wetu ndio ushindi wetu, natoa rai kuwa jukumu la kukusanya mapato ni letu sote tuhakikishe tunadhibiti uvujaji wa mapato hasa kipindi hiki cha mavuno" amesema DC Mahawe na kuongeza;
"Hakuna diwani atalalamika akose kura 2025 kwasababu mambo mengi Mh Rais amefanya katika kata yake hivyo ni wajibu wa madiwani kuwaeleza mazuri yanayofanywa na Serikali" ameeleza
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa