Mkuu wa Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, Esther Mahawe amewataka wananchi kuwekeza katika kilimo cha kahawa, parachichi na makademia kwa kuwa ni fursa ya biashara katika soko la kimataifa huku akiipongeza taasisi ya Kates Foundation kwa uwekezaji wa miti ambayo ni njia mojawapo ya utunzaji mazingira.
Mkuu huyo wa wilaya amesema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ameamua kuwekeza katika sekta ya kilimo hivyo wananchi wanatakiwa kutumia fursa hiyo.
Akizungumza wakati alipotembelea taasisi hiyo leo Jumatano Julai 19, 2023 DC Mahawe amesem kuwa wameamua kuahirisha mambo mengine yaliyopangwa kufanyika leo na kuwatembelea wadau ili kuthamini kazi wanazozifanya katika wilaya hiyo.
Taasisi hiyo imewekeza katika uzajishaji wa zaidi ya miti 200,000 ikiwemo ya matunda katika Kijiji cha Hatete kilichopo kata ya Iyula Wilayani Mbozi.
“Nianze na pongezi. Hongereni sana, tulikuwa na ratiba zingine kama kawaida Mkuu wa Wilaya huwezi kukosa ratiba kwamba kuna siku tu imekaa bila kazi. Basi tukaahirisha jambo lingine ambalo lilikuwa lifanyike leo tukaja ili kuthamini kazi inayofanywa na wadau ndani ya wilaya yetu” amesema
Amesema manufaa ya mradi huo yatakuwa ya Wilaya, Mkoa na Taifa kwa ujumla huku akigusia tahadhari ya El nino ambayo inasababishwa na uharibifu wa mazingira hivyo program hiyo inasaidia kutunza mazingira.
DC huyo ambaye alikuwa ameambatana na baadhi ya viongozi wa Hamashauri hiyo ameeleza kuwa licha ya kuuza mazao yanayotokana na kilimo hicho ipo fursa ya kuuza hewa ya ukaa ambayo katika maeneo mengine nchini wakulima wamenufaika nayo hivyo amewataka wananchi kuendelea kuwekeza katika upandaji wa miche ya parachichi, kahawa na makademia.
Amesema kuwa wakulima wakiwekeza katika kilimo hicho wataongeza kipato na kuisaidia halmashauri hiyo kuongeza mapato.
Amemshukuru Rais Samia kwa kutoa ruzuku ya pembejeo za kilimo ikiwa ni mpango wa kuwasaidia na kuwainua wakulima.
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa