• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Mbozi District Council
Mbozi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango , Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Idara ya Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mipango Miji na Maliasili
    • Vitengo
      • Wakaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Mipango na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
      • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
    • Majarida Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio

DC MAHAWE AWAITA WANAMBOZI KUJIFUNZA NANENANE MKOANI MBEYA

Kurushwa hewani: August 7th, 2023

Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Esther Mahawe ametoa wito kwa wananchi wa Wilaya hiyo na Mkoa wa Songwe kwa ujumla kushiriki katika maonyesho ya kilimo, ufugaji na uvuvi maarufu Nanenane ili waweze kujifunza mambo mbalimbali.

Amesema kuwa maonyesho hayo yana lengo la kuwapa elimu wananchi katika sekta ya kilimo, ufugaji na uvuvi hivyo watumie fursa hiyo kutokana na Wilaya hiyo kujihusisha na kilimo kwa asilimia kubwa na hakuna kiingilio.

"Niwasihi wananchi wa Mbozi na Mkoa wa Songwe kwa ujumla wafike kwenye maonyesho haya ili waweze kujifunza. Kuna mambo mengi ambayo wakifika watonufaika, maonyesho ya mwaka huu yamekuwa tofauti hivyo wakija hawataondoka bure" amesema

 

Akiwa kwenye banda la maonyesho la Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi leo Ijumaa Agosti 4, 2023 Mkuu huyo wa Wilaya ya Mbozi ambaye amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Dk Francis Michael katika maadhimisho hayo amebainisha kuwa wananchi watapata fursa ya kuona mbegu bora za mazao na mifugo, kujifunza mbinu za kilimo na ufugaji bora pamoja na kupata elimu ya mikopo ya kilimo kutoka katika taasisi za fedha.

Hata hivyo, ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi kwa maandalizi mazuri katika banda la Halmashauri hiyo ambapo kuna vitu mbalimbali ikiwemo mbegu za mazao, kuku   pamoja na bidhaa mbalimbali za mazao zinazotoka katika wilaya hiyo.

Aidha, DC huyo ametoa rai kwa wakulima kujiunga kwenye vyama vya ushirika AMCOS huku akiwatoa hofu baadhi ambao wanawasiwasi kudhulumiwa katika vyama hivyo.

"Jana Waziri Mkuu alitoa maelekezo kwa Mkoa wa Songwe kusimamia AMCOS ili kuokoa kazi za wakulima. Niseme tu kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa tayari tulishaanza kufanyia kazi maelekezo ya awali na tayati tumeshafanikiwa kusaidia Sh169 milioni kati ya Sh299 milioni zilizokiwa zimepotea kwenye mikono ya viongozi wa AMCOS 23 zimeokolewa na kazi bado inaendelea" ameeleza

Amesema kuwa bado wanaendelea kufanyia kazi maelekezo ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ili kuhakikisha fedha za wakulima kwenye AMCOS hazitumiki vibaya.

DC Mahawe amemshukuru na kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali wananchi hasa katika sekta ya kilimo

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA March 09, 2025
  • RASIMU PENDEKEZWA YA SHERIA NDOGO ZA MWAKA 2025. March 09, 2025
  • Ona vyote

Habari Mpya

  • DC MBEGA AWATAKA VIONGOZI WA KATA KUSHIRIKIANA KATIKA UTENDAJI

    March 21, 2025
  • DC MBEGA AGAWA SARE ZA SHULE KWA WANAFUNZI 120 WANAOTOKA MAZINGIRA MAGUMU ISANGU

    March 21, 2025
  • DC MBEGA AFANYA ZIARA KUSIKILIZA NA KUTATUA KERO ZA WANANCHI, ASISITIZA USHIRIKIANO KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    March 19, 2025
  • DC MBEGA ASISITIZA UIMARISHAJI NA USIMAMIZI MZURI WA AMCOS MBOZI

    March 18, 2025
  • Ona vyote

Video

VIJANA MSITUMIE MIKOPO YA 10% KUBET MBOZI
video zaidi

Kurasa za Karibu

  • You Tube
  • Katiba

Tovuti Muhimu

  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Ikulu
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

Watembeleaji wa kimataifa

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

writingMasterThesis

Eneo la ramani

Wasiliana nasi

    Mbozi

    Anuani: 3

    Simu: 025-2580272

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa