Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Mhe. Esther Mahawe ametembelea Hospital ya Vwawa kuangalia mwenendo wa matibabu yanayotolewa na madaktari bingwa kambi ya Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Mkuu huyo wa Wilaya ametembelea Hospitali hiyo leo Alhamisi Mei 16, 2024.
Akizungumza na baadhi ya wananchi walifika kupata huduma za kibingwa katika hospitali hiyo, Mhe. Mahawe amesema kuwa usipokuwa na afya imara huwezi kufanya kazi hata ikiwa na mikakati kiasi gani.
"Nichukue fursa hii kumshukuru sana Mheshimiwa Rais Samia kwa kuwaleta madaktari hawa, tangu Mheshimiwa Rais ameingia madarakani amefanya mambo makubwa sana hasa katika sekta ya afya kwa kuleta vifaa tiba ikiwemo mashine za kisasa"
"Lakini kama mmemsikiliza waziri wa afya bungeni akiwasilisha bajeti ya afya kuna ongezeko kubwa baada ya Mhe. Rais kuingia madarakani kulinganisha na ile kabla hajaingia madarakani"
"Alitambua sio watanzania wote wanaweza kwenda katika hospitali kubwa za rufaa akaona awalete madaktari bingwa wawafuate wananchi katika maeneo yao, nani kama mama. Mama Samia tunampa maua yake hii sio kwa Mbozi tu ni nchi nzima huu ni mwanzo mzuri"
Mhe. Mahawe amesema kuwa mpaka sasa madaktari hao bingwa wamewaona watu 201 ambapo wakinamama 140 na kinababa 61 katika hospitali hiyo ya Wilaya.
"Kinababa mliopo hapa ndani leo nendeni mkawape taarifa wenzenu kuja kuangalia afya zao, wanaume mna magonjwa mengi kuliko wanawake lakini mnayavumilia. Ninyi wanaume mmeumbwa kwa tope na wanawake wameumbwa kwa mifupa, kwa hiyo acheni uzembe wakutokuja kuangalia afya zenu"
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa