Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Esther Mahawe ametoa wito kwa walimu na wanafunzi ndani ya Wilaya ya Mbozi kuhakikisha wanatokomeza division zero katika mtihani wa kidato cha nne.
Ametoa wito huo leo Jumanne Septemba 19, 2023 wakati wa hafla ya ugawaji wa taulo za kike kwa wanafunzi wa kike katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi.
Amesema kuwa taulo hizo zenye thamani ya Sh15 milioni za mapato ya ndani, zitagawiwa kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari za Serikali ambapo jumla ni wanafunzi 34827.
"Kusema ukweli kazi inafanyika katika awamu ya sita chini ya kiongozi wetu Mama Samia Suluhu Hassan. Sasa hivi mnasoma katika mazingira rafiki sana madarasa yana tiles ya vioo vyoo vizuri huwezi kulinganisha kabisa na sisi tulikotoka" amesema
"Sasa ninyi leo sijui mtakuwa na excuse gani mnasoma katika mazingira mazuri.
Lakini zamani mwanafunzi wakike katika siku zile 109 anazotakiwa kuwepo shuleni karibu siku 50 alikuwa anashindwa kufika shuleni akiingia katika ule mzunguko anashindwa kuja shuleni kwasababu mazingira hayajakaa vizuri" ameeleza
Amesema kuwa kwa sasa mazingira ni mazuri hivyo wajitahidi katika masomo kuonyesha shukrani kwa Rais Samia.
"Naomba niwasisitize wenzangu katika Wilaya ya Mbozi tuhakikishe tunatokomeza divisheni ziro na four. Inawezekana sana, penye nia pana njia"
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa