Mkuu wa Wilaya ya Mbozi (DC), Esther Mahawe ameitaka familia na ndugu wa aliyekuwa
mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Mlowo wilayani Mbozi mkoani Songwe, Meshack Mwambogolo kuishi kwa upendo na mshikamano ili kuyaenzi aliyokuwa anayafanya mwenyekiti huyo.
Mwili wa Mwambogolo ambao ulikutwa umening'inia kwenye mti katika msitu uliopo kitongoji cha Iyenga Kijiji cha Shaji Kata ya Mlangali jana umezikwa leo Jumanne Aprili 25, 2023.
Akizungumza wakati wa mazishi yaliyofanyika Kijiji cha Shaji Kata ya Mlangali wilayani Mbozi, DC Mahawe amesema zipo baadhi ya familia ambazo akifariki baba migogoro inaibuka hivyo hategemei hayo kujitokeza kwenye familia na ndugu wa Mwambogolo.
"Tuendelee kuifariji familia kwa upendo na hatimaye maumivu yao yawe yameishia kwenye kaburi la baba yao, mengine yote sisi tukafanyike baraka na kimbilio kwa familia ya marehemu" amesema mkuu huyo wa wilaya ambaye ameshiriki pamoja na mamia ya wananchi katika mazishi hayo.
"Tuendelee kupendana, hivi tulivyojitokeza Mungu atuepushe na unafiki na atupe mwisho mwema, ninawapa pole sana" amesema
Jana wakati akitoa taarifa ya kifo hicho, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Theopista Mallya alisema kuwa kabla ya kujinyonga, Mwambogolo alitoa Sh118 milioni na kuziweka kwenye akaunti ya Joseph Muhume kwa ajili ya kununulia kahawa ambapo baada ya kumuingiza fedha hizo Joseph alitoroka.
Kamanda Theopista alisema kuwa Mwambogolo aliacha ujumbe ambao unaiomba familia yake imsamehe kwa uamuzi alioufanya wa kujinyonga
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa