Mkuu wa Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, Esther Mahawe ametembelea na kukagua Shule mpya ya Lutumbi Kata ya Mlowo na madarasa manne na matundu matatu ya vyoo ya Shule ya Msingi Idunda Kata ya Iyula yanayojengwa kupitia mradi wa BOOST.
Mkuu huyo wa Wilaya ambaye aliambatana na baadhi ya viongozi wa Wilaya hiyo ametembelea shule hizo leo Jumatatu Julai 17, 2023.
Akiwa katika shule ya Idunda, DC Mahawe amewaagiza viongozi na wasimamizi wa ujenzi wa madarasa hayo kuhakikisha wanakamilisha na wanakabidhi madarasa hayo Ijumaa Julai 21 mwaka huu.
"Endeleeni kusimamia kwa kushirikiana. Mko nyuma ya wakati sana. Jitahidini Ijumaa haya madarasa yakamilike" amesisitiza.
Ameutaka uongozi wa shule hiyo kuhakikisha mazingira ya shule hiyo yanakuwa safi.
"Usafi mwingine wa mazingira uendelee kwasababu tunapomleta Mkuu wa Mkoa hapa hatutaki tena matofali yaliyozagaazagaa hapa. Hakikisheni eneo lisafishwe" ameelekeza.
Shule ya Msingi Idunda iliyopo Kata ya Iyula ilipata Shilingi Milioni 106 za mradi wa BOOST kwa ajii ya ujenzi wa madarasa manne na matundu matatu ya vyoo huku Shilini Milioni 538.5 zikitolewa kwaajili ya ujenzi wa Shule mpya ya Lutumbi Kata ya Mlowo.
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa