• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Mbozi District Council
Mbozi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango , Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Idara ya Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mipango Miji na Maliasili
    • Vitengo
      • Wakaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Mipango na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
      • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
    • Majarida Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio

DC AGAWA PIKIPIKI KWA WATENDAJI KATA TISA, MBOZI

Kurushwa hewani: February 18th, 2023

MBOZI. Mkuu wa Wilaya ya Mbozi (DC), Esther Mahawe amekabidhi pikipiki tisa kwa watendaji wa kata ambazo zitawasaidia katika kutekeleza majukumu yao.


Mkuu wa wilaya huyo amekabidhi pikipiki hizo leo Ijumaa Februari 17, 2023 katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi.


Akikabidhi pikipiki hizo, mkuu wa wilaya huyo amesema kuwa usafiri huo utawarahisishia watendaji hao wa kata hizo za pembezoni kutimiza majukumu yao kwa wakati.


DC Mahawe ametumia nafasi hiyo kuwaagiza watendaji hao kwenda kuwafuatilia watoto ambao bado hawajaripoti shuleni ili waweze kujiunga na wenzao kuendelea na masomo


"Naomba sana tuungane kwa pamoja tumsaidie mama Samia (Rais Samia Suluhu Hassan) juhudi kubwa anazofanya katika kuwasaidia wananchi wake" ameagiza DC huyo.


Amekumbusha watendaji hao kuwa makini katika matumizi ya vyombo hivyo vya moto Ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi (DED) Abdallah Nandonde amezitaja kata zilizopata pikipiki hizo kuwa ni pamoja na Nambinzo, Bara, Iyula, Idiwili, Isalalo, Itumpi, Itaka, Hezya na Nanyala.


Mkurugenzi huyo amewakumbusha watendaji hao kuzitunza pikipiki hizo na wafanyie kazi walizotumwa na sio vinginevyo.


Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, George Musyani ametoa shukurani kwa Rais Samia kwa kuwajali watendaji maana wao ndio wana kazi kubwa ya kuwahudumia wananchi.


Amewataka wakatimize wajibu wao kwa kufanya kazi kwa bidii ikiwa ni pamoja na na kukusanya mapato katika maeneo yao kwa kuwa fedha zilizonunulia pikipiki zilitokana na ukusanyaji wa mapato.


Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA March 09, 2025
  • RASIMU PENDEKEZWA YA SHERIA NDOGO ZA MWAKA 2025. March 09, 2025
  • Ona vyote

Habari Mpya

  • DC MBEGA AWATAKA VIONGOZI WA KATA KUSHIRIKIANA KATIKA UTENDAJI

    March 21, 2025
  • DC MBEGA AGAWA SARE ZA SHULE KWA WANAFUNZI 120 WANAOTOKA MAZINGIRA MAGUMU ISANGU

    March 21, 2025
  • DC MBEGA AFANYA ZIARA KUSIKILIZA NA KUTATUA KERO ZA WANANCHI, ASISITIZA USHIRIKIANO KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    March 19, 2025
  • DC MBEGA ASISITIZA UIMARISHAJI NA USIMAMIZI MZURI WA AMCOS MBOZI

    March 18, 2025
  • Ona vyote

Video

VIJANA MSITUMIE MIKOPO YA 10% KUBET MBOZI
video zaidi

Kurasa za Karibu

  • You Tube
  • Katiba

Tovuti Muhimu

  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Ikulu
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

Watembeleaji wa kimataifa

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

writingMasterThesis

Eneo la ramani

Wasiliana nasi

    Mbozi

    Anuani: 3

    Simu: 025-2580272

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa