• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Mbozi District Council
Mbozi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango , Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Idara ya Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mipango Miji na Maliasili
    • Vitengo
      • Wakaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Mipango na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
      • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
    • Majarida Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio

ANZISHENI KLINIKI YA KUWABAINI VIJANA WATUKUTU MJINI MLOWO

Kurushwa hewani: November 2nd, 2023

Mkuu wa kituo cha Polisi Mlowo, John Maro amewashauri wenyeviti wa mitaa katika mji mdogo wa Mlowo wilayani Mbozi mkoani Songwe kuanzisha kliniki ya kuwabaini vijana watukutu katika mji huo.

Maro ametoa ushauri huo leo Alhamisi Novemba 2, 2023 katika kikao cha Baraza la Kata katika mji mdogo wa Mlowo cha kupitia taarifa za utekelezaji katika kipindi cha robo ya kwanza.

Akitoa elimu katika baraza hilo, amesema kuwa suala la ulinzi na usalama ni muhimu kutokana na mji huo kuwa ni mji wa kibiashara hivyo kukiwa na usalama wa kutosha watu watafanya shughuli zao kwa amani.

‘’Usalama ni kitu muhimu sana katika masuala ya kibiashara ili shughuli zetu ziweze kwenda ninashauri katika maeneo yenu tuanzishe kliniki itakayolenga kuwabaini watu watukutu ambao tutawahoji na watatupatia taarifa za wahalifu katika maeneo yao” amesema.

Mkuu wa Polisi huyo amesisitiza suala la uanzishwaji wa ulinzi shirikishi ili kuimarisha usalama katika mitaa ya mji huo mdogo huku akitoa wito kwa wamiliki wa maduka kuweka walinzi katika maduka yao.

Maro amewataka viongozi wa mila na dini kusimamia na kusisitiza suala la kutoa elimu kwa jamii kutokana na kuwepo na matukio mengi ya watu kujiua, ulawiti na ubakaji.

Akifunga kikao hicho Mwenyekiti wa Mamlaka ya mji Mdogo Mlowo, Anna Mwasaka ameliomba Jeshi la Polisi kuchunguza uwepo wa ajali nyingi katika kipande cha barabara kuanzia Karasha mpaka Mlowo mjini.

‘’Tunaomba Jeshi la Polisi mtusaidie kumekuwa na ajali za mara kwa mara katika kipande cha Karasha mpaka Mlowo stendi kitu ambacho kinasababisha kupoteza nguvu kazi kubwa ya taifa’’ amesema.

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA March 09, 2025
  • RASIMU PENDEKEZWA YA SHERIA NDOGO ZA MWAKA 2025. March 09, 2025
  • Ona vyote

Habari Mpya

  • DC MBEGA AWATAKA VIONGOZI WA KATA KUSHIRIKIANA KATIKA UTENDAJI

    March 21, 2025
  • DC MBEGA AGAWA SARE ZA SHULE KWA WANAFUNZI 120 WANAOTOKA MAZINGIRA MAGUMU ISANGU

    March 21, 2025
  • DC MBEGA AFANYA ZIARA KUSIKILIZA NA KUTATUA KERO ZA WANANCHI, ASISITIZA USHIRIKIANO KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    March 19, 2025
  • DC MBEGA ASISITIZA UIMARISHAJI NA USIMAMIZI MZURI WA AMCOS MBOZI

    March 18, 2025
  • Ona vyote

Video

VIJANA MSITUMIE MIKOPO YA 10% KUBET MBOZI
video zaidi

Kurasa za Karibu

  • You Tube
  • Katiba

Tovuti Muhimu

  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Ikulu
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

Watembeleaji wa kimataifa

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

writingMasterThesis

Eneo la ramani

Wasiliana nasi

    Mbozi

    Anuani: 3

    Simu: 025-2580272

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa