MBOZI. Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT) Mkoa wa Songwe wameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi kwa ununuzi wa mtambo wa ujenzi excavator.
Excavator hiyo iliyonunuliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi kupitia mapato ya ndani iliwasili katika ofisi za halmashauri hiyo Jumatatu Februari 27, 2023.
Pongezi hizo zimetolewa Jana Alhamisi Machi 3, 2023 wakati wa ziara ya jumuiya hiyo ya wakitembelea miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika wilaya hiyo.
Jumuiya hiyo imesema kuwa Halmashauri ya Mbozi imeubeba mkoa wa Songwe kwani mkoa huo ulikua hauna mtambo huo hivyo kupelekea miradi kuchelewa kwa kisingizio cha kukosa mtambo huo huku ikimshauri Mkurugenzi wa Malmashauri hiyo, Abdallah Nandonde kuwa makini na usimamizi madhubuti wa mradi huo ili ulete tija.
Wenyeviti wa halmashauri za mkoa huo wameahidi kuutumia kwa kukodi kwaajili ya miradi ya halmashauri zao.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, George Musyani alisema kuwa halmashauri hiyo inampango wa kununua mitambo mingine inayofanya kazi sambamba na mtambo huo.
Jumuiya hiyo imetembelea shule ya Sekondari ya Nambala iliyojengwa kwa fedha za mradi wa SEQUIP ambao jumuiya hiyo imepongeza halmashauri hiyo kwa ujenzi wa shule hiyo.
Kwa upande wake mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Abdallah Nandonde amesema kuwa mradi huo umefanikiwa kupunguza adha ya kutembea umbali mrefu wanafunzi wa vijijini jirani na shule hiyo.
"Mpaka sasa wanafunzi walikua wanatembea umbali mrefu kwenda sekondari nyingine wa kidato cha pili na tatu wameshaanza masomo katika shule hii" amesema
Jumuiya hiyo pia imetembelea shule ya sekondari Ivwanga ambapo jumuiya hiyo imepongeza ujenzi wa shule hiyo yenye jumla ya madarasa 16, na kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha hizo kwaaajili ya ujenzi wa Madarasa hayo
Hata hivyo halmashauri ya wilaya ya Mbozi imechangia milioni 50 mapato ya ndani katika ujenzi wa matundu 39 ya vyoo na miundombinu ya maji na umeme katika shule hiyo.
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa