DC PALINGO: TUKIKUTA MAZINGIRA YAMEARIBIKA UONGOZI WA KIJIJI KUCHUKULIWA HATUA.MBOZI:
Kurushwa hewani: June 5th, 2021
DC PALINGO: TUKIKUTA MAZINGIRA YAMEARIBIKA UONGOZI WA KIJIJI KUCHUKULIWA HATUA.MBOZI:
Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, John Palingo amesema kuanzia sasa akikuta kwenye Kitongoji au Kijiji ambacho kuna uharibifu wa Mazingira Uongozi wa kijiji au Kitongoji ndio watakuwa wa kwanza kuchukuliwa hatua.Mkuu wa Wilaya ametoa kauli iyo kutokana na uharibifu wa Mazingira unaofanyika kwenye chanzo cha maji cha Mantengu ambacho Serikali imewekeza Bilioni 1.5 kwa ajili kusambaza maji katika Mji wa Vwawa."Watu wengi wanaokata miti au kulima kwenye vyanzo vya maji wanafaamika na wananchi pamoja na viongozi hivyo viongozi lazima mchukue hatua kukomesha uharibifu huu" John Palingo.Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya ameagiza Idara ya Mazingira iendeleee kutoa elimu kwa wananchi juu ya athari za kuaribu mazingira.Mkuu wa Wilaya amewaongoza wananchi wa Mbozi kupanda miti 300 kwenye chanzo cha maji cha Mantengu ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Mazingira Dunian ambayo ufanyika kila Juni 5.