SONGWE. Wafanyakazi Mkoa wa slSongwe wamesema kuwa wanaunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ya kuendelea kujenga nchi kiuchumi kwa maslahi ya wananchi pamoja na wafanyakazi.
Hayo yamesemwa leo Jumatatu Mei Mosi 2023 wakati wa sherehe ya sikukuu ya wafanyakazi 'Mei Mosi' ambayo kimkoa imefanyika katika viwanja wa Shule ya Msingi Mkwajuni wilayani Songwe.
Akisoma risalavkwa niaba ya wafanyakazi katika kilele cha sherehe hizo Katibu wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Mkoa wa Songwe ambaye pia ni a mratibu wa Tucta, Lazaro William Manyama amesema kuwa tangu Rais Samia aingie madarakani wameshuhudia nia yake njema kwa wafanyakazi.
"Nukweli usiopingika kuwa tangu mama ameingia madarakani tumeshuhudia nia yake njema kwa kupandisha madaraja yalikuwa kwa muda mrefu, kulipa madai mbalimbali ya watumishi ingawa bado kuna watumishi wanadai"
"Kubwa zaidi ni kwa wafanyakazi ambao walioondolewa kazini kwa vyeti feki kurudishiwa michango yao ya mifuko ya jamii ambayo walikuwa wanachangia" amebainisha
Amesema kuwa wanaiomba Serikali iendelee kuboresha mishahara ya wafanyakazi ambayo kiuhalisia ni midogo ukilinganisha na gharama za maisha halisi.
"Sisi wafanyakazi tunaimani kuwa Serikali ikiboresha mishahara yetu itaongeza morali ya kufanya kazi mwisho tija itaongezeka" ameeleza
"Wafanyakazi tunatambua pia juhudi za kuongeza ajira kupitia sekta binafsi. Tunaipongeza Serikali na tunaunga juhudi hizo isipokuwa tunaomba ajira ziwe za staha, ziwe zinalinda uhuru, heshima na usalama wa wafanyakazi, mikataba ya ajira, kulipwa mishahara kwa wakati"
Pia wafanyakazi hao wameipongeza ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe kwa jinsi inavyoshirikiana na wafanyakazi na kutatua changamoto mbalimbali za wafanyakazi
"Tuna baadhi ya changamoto ambazo tunajua zipo ndani ya uwezo wako kama vile upandaji wa madaraja kwa mserereko, fedha za uhamisho kutolipwa kwa wakati, fedha za mizigo kwa wastaafu kutolipwa kwa wakati, upungufu wa nyumba za watumishi, wafanyakazi wa afya kutolipwa extraduty kwa wakati, wafanyakazi kusimamia miradi ya ujenzi wakati sio taaluma yao" maeeleza
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa