Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mheshimiwa Dkt. Francis Michael ametatua mgogoro wa shamba la NAFCO kati yawamiliki ambao ni Wakala wa Mbegu ASA na baadhi ya vivijiji vinavyozunguka shamba hilo.
Dkt. Michael ametatua mgogoro huo leo Alhamisi Novemba 2023 katika Kijiji cha Magamba katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe Mkuu wa Mkoa huo amesema kuwa alisikia sitofahamu hiyo na akamtuma Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Mhe. Ester Mahawe.
"Na sisi kama viongozi tumeona jinsi tunavyozidi kukaa na kuchelewa kutoa suluhisho la tatizo hili tu takuwa tunawakwaza wakulima kwasababa ni msimu wa kutayarisha mashamba kwa hiyo kama kuna mgogoro wowote wa ardhi haukupaswa kukalishwa kwa muda mrefu ili tumalize wananchi waendelee na kilimo" amesema
"Ndio maana leo nimekuja ili tuonane na hawa wananchi, migogoro imekuwa mingi ya ardhi lakini tumeitatua naamini na huu umekwisha" ameeleza
Mkuu wa mkoa huyo ametoa ekari 500 kutoka katika ekari 1,586 na kuwagawia wananchi wa vijiji hivyo vinne ambapo Kila Kijiji kitapewa ekari 125, ambapo awali vijiji vyote hivyo vilikuwa vikigombea ekari 250.
Amevitaja Vijiji vilivyopewa ekari hizo kuwa ni Magamba, Hangomba, Itewe na Iporoto.
Vilevile Mkuu wa Mkoa huyo amemuagiza Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi kuhakikisha maafisa ardhi wanakwenda kuhakiki na kupima eneo hilo ili wakulima waendelee na kilimo.
Akieleza chanzo cha mgogoro huo Afisa Ardhi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Emmanuel Mamkwe amesema kuwa ni wamiliki wa shamba la NAFCO kulalamikia mipaka ya vijiji hivyo kuingia katika shamba lao hivyo kuomba Wiraza ya Ardhi kufufua mipaka ya shamba hilo kulingana na ramani ya upimaji iliyopo wizarani.
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa