Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mheshimiwa Daniel Chongolo amewasili katika Mkoa wa Songwe kuanza majukumu yake ambapo amepokelewa katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Songwe.
Mhe. Chongolo amewasili katika ofisi za CCM Mkoa leo Jumatatu Machi 18, 2024 na kupokelewa na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe, Bi. Happiness Seneda na viongozi wa Chama wakiongozwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Songwe, ndugu ndugu said Kineng'ena
Akizungumza katika ofisi hizo za CCM Mkoa, Mhe. Chongolo amesem "Tangia juzi nilipo apa nimekuwa mjumbe wa kamati ya siasa ya Mkoa wa Songwe nimesha wasili Songwe na nipo tayari kwaajili ya kuanza kazi,
"Lakini pia nimepewa dhamana ya kuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe kwa maana ya kuratibu na kusimamia Ilani ya CCM ya 2020-2025, hivyo msiwe na wasiwasi tutajifunza wote na matokeo tutapimana mwishoni pamoja" amesema Chongolo na kuongeza;
"Kikubwa naomba ushirikiano wenuna tuseme ukweli kwa kila jambo, tukiwa wakweli tutayaona matokeo na yenye tija" amesisitiza
Baada ya kuwasili, Mhe. Chongolo anatembelea taasisi mbalimbali za Serikali katika Mkoa huo.
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa