Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Mhe. George Musyani ametembelea shule ya Sekondari ya Isandula kata ya Ukwile kushughulikia mgogoro wa ardhi katika Kijiji hicho kwa kufanya majadiliano kutafuta suluhuhisho baina ya pande mbili.
Majadiliano kuhusu mgogoro huo yamefanyika leo Jumamosi Machi 16, 2024 katika Shule ya Sekondari Isandula kata ya Ukwile.
Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti huyo wa Halmashauri amesemakuwa kuwa wamefika katika sekondari hiyo ambapo kuna mgogoro baina ya wananchi wa Kijiji Cha Rudewa na Sekondari ya Isandula
"Tumesikiliza maoni ya wananchi na pia tumekutana na Serikali ya Kijiji na Halmashauri za chama na bodi ya Shule kuweza kujua uhalisia na historia" amesema George Musyani
Ameongeza kuwa "historia inaonesha kuwa eneo hilo lilikuwa wazi mwaka 2004 Serikali ilipotoa agizo ya kujenga sekondari kila kata ndipo taratibu za uanzhishwaji wa Shule ulianza na Kijiji kilitenga ekari 125, wametufafanulia katika kikao cha ndani"
Mwenyekiti huyo amesema kuwa baada ya kikao hicho cha ndani wamerudi kuwasikiza wananchi ambao ndio wenye kero ambapo madai yao wamesema kupitia mikutano yao ya hadhara walitoa kiasi cha ekari 20 na baadaye waliwaongeza ekari kumi hivyo shule ikawa na ekari 30.
"Baada ya kuwasikiliza pande zote mbili tumeona kuna ukinzani wa taarifa katika kuhitimisha tumeona sote turudi kujiridhisha na tumempa kazi Mkurugenzi Mtendaji ayafanyie kazi baadhi ya mambo ikiwa moja wapo ni kufuatilia taarifa na mihutasari ya Kijiji cha Rudewa ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha viongozi wa kipindi hicho ili kujua mchakato wa hati ilivyotolewa"
"Tunahitaji kujua utaratibu upi ulitumika katika suala la upimaji wa ardhi wakihusishwa majirani wa eneo, na pia tutahitaji ofisi ya kijiji iweze kutuletea nyaraka tuweze kujua nani walikuwepo kama majirani Ili tujue nani anamwingilia mwenzake" ameeleza
Akisimulia historia ya eneo hilo Redson Swepa ambeye alikuwa mwenyekiti wa Kijiji Cha Chimbuya wakati huo amesema kuwa shule ya kata hiyo ilitakiwa kujengwa katika Kijiji cha Ihanda lakini viongozi wa kata hiyo waliona kama kata wawe na Shule yao kwa kuwa walikuwa
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa