Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Mhe. Hamad Mbega, amefanya kikao maalum na Kamati ya Amani ya wilaya hiyo, akisisitiza umuhimu wa mshikamano na ushirikiano kati ya Serikali na makundi mbalimbali ya kijamii.
Katika mkutano huo, Mhe. Mbega alieleza kuwa jukumu la kamati hiyo linaenda zaidi ya kulinda amani, bali pia linahusisha kuimarisha mshikamano wa kijamii, kukuza maadili na kuhakikisha maendeleo endelevu katika wilaya hiyo.
"Ninyi ni zaidi ya amani," alisema DC Mbega, akiwataka wajumbe wa kamati hiyo kuhakikisha wanakuwa mfano bora wa kuigwa kwa kuonyesha mshikamano wa dhati, uvumilivu wa kiimani na utatuzi wa changamoto kwa njia za mazungumzo.
Aliwataka kuhakikisha kila mmoja anashiriki kikamilifu katika kuhamasisha jamii kuwa na maelewano kwa manufaa ya wote.
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa