• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Mbozi District Council
Mbozi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango , Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Idara ya Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mipango Miji na Maliasili
    • Vitengo
      • Wakaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Mipango na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
      • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
    • Majarida Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio

MBOZI ILIVYONUFAIKA MIAKA 2 YA RAIS SAMIA

Kurushwa hewani: April 6th, 2023

Mbozi. Ikiwa anatimiza miaka miwili madarakani, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amedhihirisha utendaji wake katika miradi mbalimbali nchini.

Tangu aapishwe Machi 19, 2021 kushika wadhifa huo amekuwa akifanya jitihada za kuanzisha na kuendeleza miradi mikubwa ya maendeleo kwa lengo la kukuza uchumi katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Kama ilivyo katika maeneo mengine, mafanikio yamejidhihirisha katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe ambayo imenufaika na miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Mkuu huyo wa nchi ambaye ameandika historia ya kuwa Rais wa kwanza mwanamke Tanzania, ameandika historia katika miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Mbozi.

Miongoni mwa mafanikio ambayo yamepatikana ndani ya kipindi cha uongozi wake Rais Samia ni pamoja na sekta ya Afya, Elimu, Miundombinu, Kilimo na Maji.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Bw. Abdallah Nandonde anaeleza kuwa, Kati ya Julai  2020 hadi kufikia mwezi Januari 2023, jumla ya Tshs. Bilioni 16 zimepokelewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambapo kati ya fedha hizo kiasi cha shilingi bilioni 5.6 ni fedha za ndani (Ruzuku ya Serikali Kuu) na shilingi bilioni 10.3 ni fedha za wafadhili.

“Ni katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Serikali ya  awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia ndipo ujenzi wa vituo vya afya vipya vitatu vimejengwa katika wilaya hiyo ambavyo vinagharimu shilingi billion 1.3 ambavyo ni Itaka, Nambinzo na Hezya” anafafanua Bw Nandonde

Vituo hivyo vitaleta ahueni ya upatikanaji wa huduma za afya kwa wakazi wa wilaya hiyo.

Pia, shilingi milioni 500 zimetolewa kwaajili ya ukamilishaji wa Zahanati 10 ambazo ni Chizumbi, Shititi, Lusungo, Nsenga, Shilanga, Mbimba, Ipanzya, Mtunduru, Isowezya na Maninga.

Katika uongozi wake Rais Samia ambaye kabla ya kuapishwa kushika nafasi hiyo ya juu nchini alikuwa Makamu wa Rais, Serikali yake imefanikisha ujenzi wa shule mpya mbili mpya za Sekondari zenye thamani ya shilingi milioni 940 kupitia mpango wa SEQUIP. Aidha   matundu ya vyoo 26 vya wanafunzi kwa  Shule za Sekondari Mlowo na Ilolo yamejengwa kwa thamani ya shilingi  26.4 milioni.

Pia Mama samia amejenga  madarasa 146 na samani katika shule 44 za Sekondari zenye thamani ya shilingi bilioni 2.8 kupitia fedha za Mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO-19, vilevile ujenzi wa Bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalum Shule ya Msingi Lutumbi uliogharimu shilingi milioni 80, na pia ujenzi wa madarasa 37 na matundu ya vyoo 271 katika Shule 38 yenye Zaidi ya  thamani ya shilingi milioni 904

Pia, kipindi cha miaka miwili cha serikali ya awamu ya sita wananchi wamenufaika kupitia mikopo ya asilimia 10 zinazotolewa na serikali kiasi cha Zaidi ya bilioni  1.2  kwa vikundi 213 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Hata hivyo baadhi ya miradi inayotekelezwa kwa fedha za mapato ya ndani ni pamoja na ununuzi wa mtambo wa barabara wenye thamani ya milioni 500, ukamilishaji wa Kituo cha Afya Halungu milioni 400, ukamilishaji wa zahanati ya Mbimba na Nambala milioni 40, kuwezesha ujenzi wa maegesho ya magari Vwawa milioni 74, ununuzi wa mashine ya kufyatua tofali milioni 29.7.

Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri George Musyani amesema kuwa halmashauri hiyo inampango wa kununua mitambo mingine ya kutengenezea barabara inayofanya kazi sambamba na mtambo huo.

‘’Kupitia  mapato ya ndani halmashauri yetu inampango wa kuongeza mitambo mingine inayofanyakazi sambambamba na mtambo huo ’’ alisema Musyani

Ili kuimarisha sekta ya kilimo katika Wilaya ya Mbozi, Machi 10, 2023 Serikali inayoongozwa na Rais Samia imegawa pikipiki 81 kwa maofisa ugani wa Wilaya hiyo.

Katika ugawaji wa pikipiki hizo, Mkuu wa Wilaya hiyo, Esther Mahawe alisema amesema kuwa wilaya ya hiyo inakwenda kufanya mapinduzi makubwa katika sekta ya kilimo baada ya maafisa ugani kukabidhiwa pikipiki na Serikali.

DC Mahawe alisema anaamini kama wilaya inakwenda kuzalisha kwa wingi kutokana na wataalamu wa kilimo kuwezeshwa vitendea kazi ambavyo vitawafanya wamfikie mpaka mkulima wa chini huku alimpongeza Rais Samia kwa kuwapatia vyombo hivyo ambavyo vitakwenda kuinua utendaji wa maofisa hao.

"Hata kama watu wanasema hawajaona kama vitu vinafanyika, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni mama anaupiga mwingi mpaka unamwagika" alisema DC huyo na kuongeza

Tumeona kwa macho yetu juhudi za mama kwaajili ya kuwezeshwa kilimo cha kisasa chini ya Waziri wake wa Kilimo, Bashe. Niwahimize muende mkafanye kazi ndugu zangu mkaoneshe kabla ya kupata pikipiki ilikuaje na baada ya kupata imekuaje" alisema

Akiwa kwenye ziara katika Wilaya ya Mbozi, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa Majaliwa alibainisha kuwa

ili kuwapa motisha wakulima wakiwamo wa Wilaya hiyo, Serikali imetoa ruzuku kwenye pembejeo za kilimo ikiwemo mbolea hali ambayo itawasaidia wananchi wakowemo wa Wilaya ya Mbozi wapate pembejeo kwa urahisi.

Waziri Mkuu huyo aliwasisitiza wananchi wa Mbozi kulima zao la kahawa kwa kuwa zao hilo ni la mkakati na muhimu

Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi katika kipindi cha Uongozi wa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepata mafanikio makubwa hususani katika Nyanja za Sekta ya Elimu, Afya na uwezeshaji wananchi kiuchumi kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF III) na ukusanyaji wa mapato ya ndani ambapo asilimia 40 ya fedha za makusanyo imekuwa ikipelekewa kwenye kuchangia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo utoaji wa mikopo kwa Vikundi vya akina mama, Vijana na watu wenye Ulemavu.

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA March 09, 2025
  • RASIMU PENDEKEZWA YA SHERIA NDOGO ZA MWAKA 2025. March 09, 2025
  • Ona vyote

Habari Mpya

  • DC MBEGA AWATAKA VIONGOZI WA KATA KUSHIRIKIANA KATIKA UTENDAJI

    March 21, 2025
  • DC MBEGA AGAWA SARE ZA SHULE KWA WANAFUNZI 120 WANAOTOKA MAZINGIRA MAGUMU ISANGU

    March 21, 2025
  • DC MBEGA AFANYA ZIARA KUSIKILIZA NA KUTATUA KERO ZA WANANCHI, ASISITIZA USHIRIKIANO KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    March 19, 2025
  • DC MBEGA ASISITIZA UIMARISHAJI NA USIMAMIZI MZURI WA AMCOS MBOZI

    March 18, 2025
  • Ona vyote

Video

VIJANA MSITUMIE MIKOPO YA 10% KUBET MBOZI
video zaidi

Kurasa za Karibu

  • You Tube
  • Katiba

Tovuti Muhimu

  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Ikulu
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

Watembeleaji wa kimataifa

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

writingMasterThesis

Eneo la ramani

Wasiliana nasi

    Mbozi

    Anuani: 3

    Simu: 025-2580272

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa