MBOZI. Mwenyekiti Bodi Hifadhi ya Ngorongoro, Jenerali Venance Mabeyo amesema makumbusho ya kisasa katika eneo la kimondo Kijiji cha Ndolezi kata ya Mlangali wilayani Mbozi mkoani Songwe yatafungua fursa za kiuchumi katika jamii hiyo.
Mabeyo amesema hayo leo Jumamosi Machi 4, 2023 wakati akifungua makumbusho hayo.
Katika hotuba yake Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama mstaafu huyo amesema sio jambo dogo Kijiji hicho kupata makumbusho hayo ya kisasa.
Mabeyo amewashukuru viongozi wa kimila kutoa ushirikiano kuonesha mila na desturi ya jamii inayokaa katika maeneo hayo na kusema kua makumbusho hayo ni ya kwanza Nyanda za Juu Kusuni.
"Kuna baadhi walikua wanaogopa kufika hapa lakini kwa sasa panafikika, nawashukuru vijana wazalendo waliokuja na wazo hili la kuanzisha makumbusho haya" amesema na kuongeza
"Kilichotokea hapa ni cha kuigwa kwasababu ni fursa ambayo itawaongezea wanajamii wanayoizunguka kipato kupitia suala la utalii"
Ameitaka jamii kutunza eneo hilo kutokana na historia yake, akieleza kuwa hata jina la mkoa wa Songwe umetokana na uwepo wa ndege wakubwa wenye shingo ndefu walioitwa Songwesis.
Hata hivyo ameahidi kulifanyia kazi suala la fidia ya maeneo yao na kuahidi kuwa litafanyiwa kazi kwa muda mfupi kwa kuwa Serikali ni sikivu.
"Serikali haiwezi kushindwa kulipa bilioni 1.4 kwa wananchi waliopisha utanuzi wa kituo hiki naomba muendelee kuipenda selikali yenu" amesisitiza
Ameiagiza Hifadhi ya Ngorongoro kuendelea kubuni vivutio vingi katika eneo hilo na kuongeza kuwa watalii wakija eneo hili wakute vitu vingi vya kutembelea.
Mabeyo amesema kuwa faida ya kutembelea vivutio vya utalii ni pamoja na kupata afya ya akili huki akiwasihi wasiache kuboresha shule zilizopo katika eneo hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Dk Fransis Michael ameikaribisha Hifadhi ya Ngorongoro kufanya maboresho zaidi katika kituo cha kimondo.
Amezitaja fursa za uwekezaji katika eneo la maliasili na utalii katika mkoa huo kuwa ni pamoja na ujenzi wa hoteli kubwa pamoja na kumbi za mikutano, kampuni za kitalii, campsite eneo la kimondo, ufugaji nyuki, bandari kavu, utalii wa madini na utalii wa kilimo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbozi (DC), Esther Mahawe amesemakuwa Kila jambo jema linakuja na maumivu kidogo hivyo hiki kinachojengwa kitaleta tija hivyo wanajamii wakipokee kwa
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa