Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Mhe. Hamad Mbega ameongoza Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi pamoja na baadhi ya Wakuu wa Idara za Halmashauri ya Wilaya hiyo katika ziara maalumu katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kwa lengo la kujifunza mbinu bora za kuongeza ukusanyaji wa mapato pasipokutegemea mazao ya kilimo.
Ziara hiyo imefanyika leo Jumatatu Februari 24, 2025 ambayo imelenga kuboresha utendaji wa Halmashauri kwa kuiga mifano bora ya usimamizi wa ukusanyaji wa mapato.
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke imekuwa na mafanikio katika usimamizi na ukusanyaji wa mapato kwa kutumia mifumo ya kidijitali na mbinu za kisasa hasa kuanzishwa kwa Cluster (kanda 06 za ukusanyaji wa mapato).
Katika ziara hiyo, Kamati hiyo ilipata fursa ya kujifunza namna ya kuimarisha vyanzo vya mapato vinavyotokana na sekta zisizo za kilimo kama leseni za biashara, vibali vya ujenzi, service levy n.k
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke Mhe. Abdallah Mtinika amesema kuwa Manispaa hiyo ndio inaongoza kwa ukusanyaji wa mapato Mkoa wa Dar es salaam ambapo mwaka 2023/2024 walikusanya mapato ya ndani kwa asilimia 100 na kwa mwaka wa fedha 2024/2025 hadi kufikia Disemba, 2024 Manispaa ilikuwa imekusanya mapato yake ya ndani kwa asilimia 58.
Mstahiki Meya aliongeza kuwa katika Mwaka wa fedha 2025/2026 Manispaa imejiwekea lengo la kukusanya Tshs 63 Bilioni.
Katika kikao hicho Meya huyo alibainisha kuwa Manisipaa ya Temeke ilivyofanikiwa kuongeza mapato kwa asilimia 30 kupitia uboreshaji wa mfumo bora wa ukusanyaji pamoja na kuongeza nguvu kazi ya wakusanyaji mapato na vyombo vya usafiri vinavyowafanya kupenya kila mahali kwaajili ya kufutilia mapato.
Aidha katika ziara hiyo Kamati ilifanikiwa kutembelea maeneo mbalimbali ikiwemo ujenzi wa Hospitali ya Mbagala Rangitatu na Klasta ya ukusanyaji wa mapato Charambe na kujionea jinsi mapato yanavyokusanywa moja kwa moja bila mianya ya upotevu wa fedha
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa