Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Mhe. Hamad Mbega amefuturisha viongozi pamoja na makundi mbalimbali ya kijamii huku akitoa rai kwa wananchi kuendelea kudumisha amani, upendo, umoja na kutenda matendo mema kama wanavyotenda kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu na Kwaresma.
Mhe. Mbega ameandaa hafla hiyo iliyofanyika Jumapili Machi 16, 2025 ambapo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, Taasisi za Serikali, Taasisi binafsi, viongozi kutoka madhehebu mbalimbali ya dini, Kamati ya Amani Wilaya na wawakilishi wa makundi mbalimbali ya kijamii ya Wilaya hiyo.
Akizungumza wakati wa Iftari hiyo, DC Mbega amewataka wananchi kutumia mfungo wa Mwezi Mtukufu na Kwaresma kuendelea kuliombea Taifa na Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa