Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Mhe. Hamadi Mbega amewataka wananchi wanaokata miti bila kuwa na vibali wakiwemo wanaochoma mkaa kuacha mara moja tabia hiyo kwani watakaobainika watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
Mhe. Mbega ametoa agizo hilo leo Jumanne Machi 04, 2025 wakati wa operesheni maalumu ya kukabiliana na watu wanaoharibu mazingira kwa kukata miti kwa ajili ya uchomaji mkaa inayofanyika katika Wilaya ya Mbozi.
Akiwa katika operesheni hiyo, DC Mbega ambaye aliambatana na Kamati ya Usalama ya Wilaya, Wataalamu kutoka Idara ya Maliasili na Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi pamoja na wataalamu kutoka TFS, amesema kuwa ukataji miti kwa ajili ya uchomaji mkaa umekuwa tatizo ambalo linasababisha uharibifu mkubwa wa mazingira.
Katika operesheni hiyo ambayo ilikuwa ni utekelezaji wa maagiro ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Daniel Chongolo aliyoyatoa, jumla ya pikipiki 10
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa