Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Mh. Esther Mahawe amewataka madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi kwenda kusimamia kwa dhati miradi ya maendeleo katika maeneo yao.
Rai hiyo ameitoa leo Alhamisi Disemba 7, 2023 wakati wa Baraza Maalumu la Madiwani lililolenga kuchukua hatua dhidi ya waliotajwa katika hoja za CAG kwaajili ya kutekeleza agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alilolitoa wakati wa ziara yake Wilayani humo mwezi Novemba.
"Madiwani naomba muwe na umiliki wa miradi hiyo, na pia fanyeni mikutano ya hadhara katika maeneo yenu kuwaelezea wananchi aina ya mradi ulioletwa, gharama yake na unakwenda kuwanufaisha vipi wananchi"
"Madiwani wengi hawafanyi mikutano ya hadhara hata kuelezea kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya awamu ya sita. Waheshimiwa madiwani na wabunge wetu jitahidini sana kuwafikia wananchi wenu mapema mkaeleze mema yanayofanya na mheshimiwa Rais"
Ameongeza kuwa; "Wilaya ya Mbozi inapokea miradi mingi ya afya, elimu, maji miundombinu lakini nani ataielezea kama sio ninyi, kazi hii imeachwa kwa wateule wa Rais tu wakati wote ni wajibu wetu kufanya haya" ameeleza
"Tunaomba sana usitajwe hata kama unauza vifaa na Kuna uchunguzi unafanywa kama Kuna madiwani wangapi wanajihusisha katika miradi ambayo mwishowake imeleta shida"
Tukimaliza huo mchakato tutakuja na majibu jinsi gani na ninyi mmekua sehemu ya kuharibu michakato ya manunuzi na kuwatishia watumishi usipo nipa hivi nitakuazimia"
Amewataka madiwani hao kuwapa ushirikiano watumishi walioletwa ili wafanyekazi kwa amani na si kuogopa kuazimiwa.
"Lakini Halmashauri kupitia madiwani na watumishi simamieni mapato Halmashauri hii kuna mapato mengi yanavuja, tunadai manispaa na mji lakini mapato yapo chini wakusanyaji ni ninyi"
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa