Mkuu wa Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe , Mhe. Esther Mahawe amekutana na kuzungumza na wadau wa kilimo cha kahawa Wilayani Mbozi.
DC Mahawe amekutana na wadau hao leo Jumanne Septemba 26, 2023 katika Ukumbi wa Kanisa la Morovian mjini Vwawa.
Kikao hicho ambapo pia kilihidhuriwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mbozi, George Musyani, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Mbunge wa Jimbo la Mbozi, George Mwanisongole na wadau mabalimbali kimejadili mikakati mbalimbali ambayo itasaidia zao la kahawa kuwa na tija.
Akizungumza katika kikao hicho, Mkuu huyo wa wilaya amesema kuwa miongoni mwa mikakati inayofanyika ni pamoja na kuwakutanisha wakulima wa kahawa na kampuni ya kuvuna carbon kutoka kwenye kahawa ambapo kupitia kampuni hiyo wakulima watajiongezea kipato.
Pia, DC Mahawe amesema mkakati mwingine ni kuzidi kutoa elimu na hamasa kwa wanawake kuingia zaidi kwenye uzalishaji wa zao hilo huku akiwasihi wanaume kuwaruhusu wake zao kwa kuwa itasaidia kuleta maendeleo katika familia.
Amesema kuwa kama wakulima wataongeza kipato kupitia zao hilo hata Halmashauri nayo itaweza kukukusanya mapato zaidi.
Mkuu huyo wa Wilaya amesema kuwa Wilaya haijawaacha wakulima hao na inatafuta kila namna ili kusaidia wakulima waweze kunufaika na kilimo hicho
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa