TUNAKWENDA KUSHINDANA KIJIJI, KATA NA HALMASHAURI KWENYE USAFI WA MAZINGIRA, Dkt. NYEMBEA.
MBOZI: Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Dkt. Hamad Nyembea amesema ili kuboresha usafi wa Mazingira kwenye vijiji, Kata na Halmashauri kutakuwa na ushindani kwa Kata na Halmashauri ambao kaya au Taasisi zao zitafanikiwa kwenye vyoo bora, usafi wa mazingira na zawadi itatolewa kwa mshindi."Kata itashindanisha vijiji vyake, Halmashauri itashindanisha Kata zake na Mkoa utashindanisha Halmashauri zake na zawadi zitakuwepo nzuri ambazo zitatoa motisha kwa kazi nzuri" Dkt. Hamad Nyembea.Dkt. Nyembea amesema ayo wakati wa mafunzo kwa waheshimiwa Madiwani wa Mbozi juu ya usafi na Mazingira Kampeni inayoendeshwa na Mkoa kwa ufadhili wa UNICEF ikiwa na lengo kuwa ifikapo Juni 2023 kaya na Taasisi zote za Mkoa ziwe na vyoo bora, vifaa vya kunawia mikono kwa maji tiririka na sabuni.Dkt. Nyembea amesema elimu itatolewa kupitia kamati za Kata na vijiji ili waweze kuwafundisha wananchi juu ya choo bora.
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa