• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Mbozi District Council
Mbozi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango , Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Idara ya Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mipango Miji na Maliasili
    • Vitengo
      • Wakaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Mipango na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
      • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
    • Majarida Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio

SONGWE KUUNDA KIKOSI KAZI KUONGEZA WANACHAMA WA CHF

Kurushwa hewani: November 17th, 2020

SONGWE KUUNDA KIKOSI KAZI KUONGEZA WANACHAMA WA CHF

Uongozi wa Mkoa wa Songwe umejipanga kuunda kikosi kazi cha kuhamasisha makundi mbalimbali ya jamii kama vile Bodaboda, Mama ntilie, waliopo  kwenye vyama kama SACOS pamoja na makundi mengine kujiunga na Bima ya Afya ya Jamii iliyoboreshwa (CHF) hili kuweza kuongeza wanachama zaidi 25% kutoka 1.6% iliyopo sasa ifikapo Disemba 2020.

Hayo yamebainishwa na Katibu Tawala Mkoa wa Songwe, Dr. Self Shekalaghe wakati wa kikao kazi na watumishi  wanaohusika na uandikishaji wa CHF iliyoboreshwa, wadau wa Afya, Makatibu wa Afya pamoja na Waganga wakuu wa Halmashauri kilichofanyika ukumbi wa Vwawa Sekondari, 17 Novemba 2020.

Katibu Tawala Mkoa wa Songwe, Dr. Self Shekalaghe amesema kwa sasa Mkoa kitaifa uko nafasi ya 24 katika uandikishaji wa CHF na tumefika 1.6% tu sawa na Kaya 3,300 ambazo zimeandikishwa wakati lengo la Kitaifa ni kila Mkoa ufike 30% ya kuandikisha wanachama wa CHF. 

“Pamoja na kuunda kikosi kazi cha kuhamasisha makundi mbalimbali tunatafuta wadau mbalimbali waweze kutusaidia kufikia lengo kama ambavyo shirika la HIMSO limetusaidia usafiri wa Pikipiki ambazo watapewa waratibu kila Wilaya hili kuhakikisha uandikishaji wa wanachama wa CHF  unaongezeka” Katibu Tawala Mkoa, Dr. Shekalaghe.

Katika kuongeza asilimia za wanachama wa CHF Shirika la HIMSO limechangia pikipiki 4 zenye thamani ya shilingi Milioni 27.1 kwa ajili ya Halmashauri ya Songwe, Ileje, Momba na Tunduma.

Wakati huo huo Katibu Tawala wa Mkoa, Dr. Shekalaghe amesema  pikipiki zilizotolewa na Shirika la HIMSO atazigawa kwa Halmashauri husika baada ya kutimiza malengo ambayo watawekeana ya uandikishaji wa wanachama wa CHF kwa muda wa wiki 2 ndio watapewa kwa waliotimiza malengo tu.

Kujiunga na CHF kwa kaya ni Shilingi 30,000 ambayo utaweza kutibiwa katika Zahanati, Vituo vya Afya, Hospitali za Wilaya pamoja na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ndani ya Mkoa wa Songwe tu.

Ikumbukwe Katika CHF ya zamani kufikia Desemba 2018 Mkoa wa Songwe umekuwa kinara kitaifa kwa 76.4% na kufanikisha kaya 198,376 kujiunga na CHF ya zamani

 

   

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA March 09, 2025
  • RASIMU PENDEKEZWA YA SHERIA NDOGO ZA MWAKA 2025. March 09, 2025
  • Ona vyote

Habari Mpya

  • DC MBEGA AWATAKA VIONGOZI WA KATA KUSHIRIKIANA KATIKA UTENDAJI

    March 21, 2025
  • DC MBEGA AGAWA SARE ZA SHULE KWA WANAFUNZI 120 WANAOTOKA MAZINGIRA MAGUMU ISANGU

    March 21, 2025
  • DC MBEGA AFANYA ZIARA KUSIKILIZA NA KUTATUA KERO ZA WANANCHI, ASISITIZA USHIRIKIANO KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    March 19, 2025
  • DC MBEGA ASISITIZA UIMARISHAJI NA USIMAMIZI MZURI WA AMCOS MBOZI

    March 18, 2025
  • Ona vyote

Video

VIJANA MSITUMIE MIKOPO YA 10% KUBET MBOZI
video zaidi

Kurasa za Karibu

  • You Tube
  • Katiba

Tovuti Muhimu

  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Ikulu
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

Watembeleaji wa kimataifa

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

writingMasterThesis

Eneo la ramani

Wasiliana nasi

    Mbozi

    Anuani: 3

    Simu: 025-2580272

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa