Soko la Vwawa kujengwa kisasa kuanzia 1 September hadi 30 october 2018, litajengwa na wafanyabiashara wa soko la Vwawa kwa usimamizi wa Halmashauri.
Soko jipya la vwawa litakuwa na vyumba vya ukubwa sawa, eneo la maegesho ya magari, kisima cha maji safi, mfumo wa maji, barabara za kutosha gari kupita, vyoo vya kutosha tofauti na hali ya sasa kwani vibanda vimepishana, hakuna maji, hakuna barabara, hakuna maegesho ya magari na hakuna mpangilio ulio sahihi, hali ambayo ni hatari kwa mali za wafanyabiashara na usalama wao.
“Soko hilo linategemea kunufaisha zaidi ya wafanyabiashara 264 wa soko, kila mfanyabiashara ambaye alikuwa anafanya biashara ndani ya soko la Vwawa atapata sehemu ya kufanyia kazi” Mwenyekiti wa Halmashauri Elick Ambakisye.
Wafanyabiashara wa soko la vwawa kwa sasa wanaamia katika soko la ichenjezya kwa kipindi cha miezi 2
Makubalinao hayo yameafikiwa siku ya Ijumaa 10 August baada ya mkutano wa wafanyabiashara wa soko la vwawa na serikali ya Halmashauri ya Mbozi.
Akitoa ufafanuzi juu ya namna soko litakavyojengwa mwenyekiti wa halamshauri mhe. Elick Ambakisye amesema kabla ya kufika muafaka ni njia ipi sahihi itafaa katika ujenzi wa soko walitembelea masoko ya Mkoa wa Mbeya ili waweze kujifunza.
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa