IGANYA NI KIJIJI CHENYE MAFANIKIO KUPITIA TASAF
kijiji cha Iganya kilichopo kata ya Magamba Halmashauri ya Mbozi ni kati ya vijiji 80 vinavyonufaika na mpango wa TASAF na kimekuwa ni moja ya kijiji chenye mafanikio kupitia TASAF III.
Tangu TASAF ianze kwenye kijiji cha Iganya zaidi ya Jumla ya shilingi milioni mia moja na milioni mbili (102,732,000) zimeweza kutumika kunusuru maisha ya kaya 153 ambazo zipo kwenye mpango wa TASAF III. Kiasi cha pesa hizi kimechochea maendelo katika kijiji cha Iganya na kuwafanya wanufaika wa TASAF waone tumaini jipya kwenye maisha yao, na aya ndio mafanikio yaliyopatikana kupitia TASAF III.
Mafanikio katika kilimo, Msimu wa kilimo Kwa mwaka 2018/2019 wanufaika wa TASAF wapatao 153 kila mmoja aliweza kulima zaidi ya ekari 2 za mahindi na maharagwe kiasi cha kufanya wanufaika waweze kufikisha lengo la kuweza kulima zaidi ya ekari 300 za mahindi na maharagwe pamoja na kufanikiwa kufuga mifugo kama Mbuzi, Kuku na Ng’ombe. Hali hii ya wanufaika wa TASAF kuweza kulima zaidi ya ekari 300 imewafanya wanufaika 153 wa TASAF kuwa na uhakika wa usalama wa chakula katika kaya zao.
Wakati kabla ya TASAF kaya hizi zilikuwa hazina uhakika wa chakula katika kaya au mahali ambapo walikuwa wanaishi.
Mafanikio katika elimu, baada ya mpango wa TASAF kuingia kijiji cha Iganya mwaka 2015, wanafunzi wapatao 57 waliweza kufanikiwa kupata elimu zao, wanafunzi 21 wako katika elimu sekondari, wanafunzi 4 wako katika vyuo vikuu Tanzania na wanafunzi 22 wapo katika elimu msingi wakiendelea kupata elimu baada ya kaya zao kuingia kwenye mpango wa TASAF III.
Mafanikio katika afya, kaya zilizo kwenye mpango wa TASAF III waliweza kuwapeleka watoto wao kwenye kliniki ya watoto ili kufuatilia makuzi ya watoto wao, kwani awali walishindwa kufanya kutokana na hali ya umasikini uliokithiri pamoja na zahanati ya jirani kuwa umbali wa KM 10 kutoka kijiji cha Iganya.
Awali watoto hawa kabala ya mpango wa TASAF III kuingia kijijini walikuwa wanasumbuliwa na maradhi mbalimbali, baada ya kaya za watoto kuingia kwenye mpango wa TASAF III waliweza kujiunga na bima ya afya ya jamii na kuwa na uhakika wa nauli za kufika kwenye zahanati ya jirani kwa ajili ya matibabu kwa watoto.
Kabala ya TASAF III kijiji cha Iganya kilikuwa na watoto wengi wanaosumbuliwa na ugonjwa wa utapilamlo hali iliyokuwa inapelekea vifo kwa watoto, lakini baada ya TASAF III kuingia kijiji cha Iganya kaya kuwa na uwezo wa milo 3, kuweza kumudu gharama za matibabu, vifo vitokanavyo na ugonjwa na ugonjwa utapilamulo kwa watoto imekuwa historia kwa kaya zilizopo kijiji cha Iganya.
Mafanikio katika kiuchumi, kaya zote hizi 153 zimeweza kufanikiwa kujenga nyumba zao za kuishi wao na familia zao pamoja kupiga bati, tofauti na awali kabla ya mpango wa TASAF III kuingia kijijini walikuwa hawawezi/hawana ndoto za kumiliki nyumba zao wenyewe.
Mafanikio katika jamii, Wanufaika wa TASAF wamekuwa chachu ya maendeleo katika mambo ya maendeleo kwenye kijiji chao na mara nyingi ndio wamekuwa wakiitikia mikutano inayoitishwa na serikali na kuweza kuchahngia kwenye mambo ya maendeleo iwe ni mawazo au pesa basi huwa wanajipapasa kwa chochote kile kwa ajili ya kuijenga Iganya yao na Halmashauri ya Mbozi.
Kitendo cha kaya zilizo kwenye mpango wa TASAF III kufanikiwa kwenye kilimo, ufugaji na kuweza kumiliki nyumba zao, kimechochea wanakijiji wengi wa Iganya kuona maendeleo yao yanawezekana kwa kufanya kazi.
Serikali ya kijiji cha Iganya kupitia kwa mtendaji na mwenyekiti wamekuwa chachu kubwa kuwasaidia wanufaika wa TASAF kufika malengo yao ya kujikwamua kiuchumi kwani seriakli yao mara kwa mara imekuwa ikiwapitia kabla ba baada ya kuchukua pesa za TASAF kuona kama wanazitumi kwa kufuata maelezo ambayo wanapewa na watalamu ili waondokane na umasikini walionao.
Mratibu wa TASAF III wa halmashauri ya Mbozi, Melania kwai amesema mpango wa TASAF umefikia kaya ambazo kweli zilikuwa na mahitaji, kwa kaya ambazo zimefikiwa Mbozi ni 9936 zipo ambazo walikuwa hawana makazi TASAF III imewawezesha kupata makazi, zipo ambazo zilikuwa hazina uhakika wa chakula TASAF III imewawezesha uhakika wa chakula, zipo ambao walikuwa hawana uwezo wa kumudu gharama ya matibabu TASAF III imewawezesha uhakika wa matibabu kwa kuwawezesha kujiunga na bima ya afya ya jamii, kwani kwa 2017/2018 kaya 7018 zimeweza kulipia bima ya aya ya jamii kati ya kaya 9936 ambazo zipo kwenye mpango wa TASAF III.
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa