DC PALINGO: MAENDELEO TULIYOPATA MBOZI WANANCHI WAMECHANGIA NGUVU ZAO.
Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Mhe. John Palingo amesema maendeleo ambayo yanaonekana Mbozi yamechangiwa sana na nguvu ya wananchi katika kujitolea kwenye maendeleo.Palingo ameeleza kuwa hana shaka na wananchi wa Mbozi kwani kujitoa kwao sio tatizo bali wanayumbishwa tu na miruzi mingi na kuwavuruga hali ambayo wanashindwa waelekee wapi katika kuchangia shughuli za maendeleo."Kuchangia shughuli za maendeleo hakuepukiki na hii ni Tanzania nzima sasa inapokuja kauli kwamba wananchi wasichange ni kuwachanganya wananchi, ni kweli jukumu la Serikali ni kutoa huduma kwa wananchi lakini rasilimali ni chache na Nchi ina vipaombele vingi sana" Mhe. John Palingo.Aidha Mkuu wa Wilaya ameeleza kuwa kama Serikali imetoa fedha ya ukamilishaji wa chumba kimoja na Shule ina vyumba 5 ni jitihada zetu kusaidiana na Serikali kukamilisha vingine ili kuwasaidia wanafunzi ambao wanakaa 200 kwenye darasa moja.Mkuu wa Wilaya ametoa wito kwa Madiwani kuwaelimisha wananchi njia sahihi ya kuchangia shughuli za maendeleo ili Mbozi iweze kufika.
Mbozi
Anuani: 3
Simu: 025-2580272
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz
Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa