• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Mbozi District Council
Mbozi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango , Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Idara ya Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mipango Miji na Maliasili
    • Vitengo
      • Wakaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Mipango na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
      • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
    • Majarida Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio

BARAZA LA WATOTO LAUNDWA MBOZI KUPIGANIA HAKI ZAO

Kurushwa hewani: June 8th, 2019


Na: Baraka Mwashambwa

 

Halmashauri ya Mbozi imeeunda baraza la wilaya la watoto kwa kushirikiana na shirika la Savethechildren, baraza limeundwa kwa kushirikisha watoto kutoka katika kata zote 29 za wilaya ya Mbozi, ambazo kila kata imetoa wawakilishi wawili katika shule za msingi na sekondari.

Viongozi waliochaguliwa kuongoza baraza la watoto kwa kipindi cha miaka 2 ni, Mwenyekiti wa baraza, Shua Nzowa kutoka kata ya Shiwinga shule ya sekondari Shiwinga kidato cha II, Makamu mwenyekiti kutoka Kata ya Mlangali,  Ales Halele shule ya sekondari Mlangali kidato cha II, Katibu ni Julius Moses shule ya msingi Bara darasa la 7 kutoka kata ya Bara na Mtunsa hazina ni Suzaly Mwasenga shule ya sekondari Iganduka kidato cha 1 kata ya Msia.

Akiongea na Baraza la watoto, Afisa maendeleo ya jamii wilaya, Bi, Melania Kwai amesema kuunda kwa baraza ni kwa mujibu wa mkataba wa kimataifa wa 1989 pamoja na sera ya maendeleo ya mtoto ya 2008 ambazo zote kwa pamoja zimeelekeza kuweza kuunda kwa baraza la watoto.

Bi, Melania Kwai amewataka watoto ambao wamepata fursa ya kuwawakilisha wenzao waweze kufanya kazi ya kusimamaia haki za watoto ambao wapo katika maeneo ikiwa na  kuwatembelea watoto wenye shida mbalimbali, pamoja na kuhakikisha wanatumia vizuri sehemu ambazo wanakutana  kwenye michezo au darasani waweze  kutoa elimu juu ya haki za watoto.

“kwa sababu watoto nyie munafamiana vizuri yupi mwenye shiuda kuliko sisi  wazazi/walezi hivyo tunawaomba muweze kuwatembelea na kujua matatizo yao ikiwa na pamoja na kuripoti matukio yale ambayo yanavunja haki za watoto kisha kuwasilisha kwenye vyombo husika, kwa kufanya hivyo mutakuwa mumewasaidia watoto wengi” Bi, Melania Kwai.

Pia, Bi. Melania Kwai amelisisitiza baraza la watoto kwenda kuwaelimisha watoto kupata vyeti vya kuzaliwa ili wapate haki yao ya kulinda jina kwani vyeti hivyo vipo na vinatolewa mda wote katika ngazi ya kijiji, kata na wilaya.

 Hidaya Haonga, mratibu wa ulinzi, haki na utawala kwa watoto kutoka shirika la savethechildren amesema shirika linafanya kazi kwa kushirikiana na serikali katika kuiwezesha kwenye maeneo ya watotot, ukiona sense ya 2012 inaonyesha nusu ya watanzania nia watoto na kundi hili limekuwa linasaulika kwenye mambo yake ya mhimu kama vile haki zake na kutengewa bajeti kwa upande wa serikali, ndio sababu iliyotupelekea kuunda mabaraza ya watoto kuanzia ngazi ya kijiji, kata na hatimaye leo tunaunda la wilaya.

Afisa mipango wa Halmashauri ya Mbozi, Bw. Elasto Mwasanga  amesema halmashauri itajitahidi kuakikisha baraza la watoto  linakuwa endelevu na hai kwa kuhakikisha baraza hilo linafanya vikao vyake kila robo kwa kushirikiana na idara ya maendeleo ya jamii na savethechildren.

Atu Dzombe afisa maendelo ya jamii, anasema moja ya jukumu ambalo baraza la watotot litakwenda kufanya ni kuhakikisha wanatoa elimu ya kwa watotot wenzao jinsi ya kuwaheshimu wazazi/walezi, waalimu,  jamii na kueshimiana wao kwa wao ili kulifanya baraza la watoto liwe mfano katika ngazi ya jamii.

Mwenyekiti wa baraza la watoto wilaya, Shua Nzowa ambaye ni mwanafunzi wa shule ya sekondari shiwinga amewataka watoto wenzake ambao wanaunda baraza la watoto pamoja na wale ambao wanawaakilisha huko kwenye kata zao kutoa ushirikiano kwa wazazi/walezi ambao kwa apmoja wameamua kuunda kwa baraza la watoto ili kuweza kutatua changamoto mbalimbali ambazo sisi watoto tunakumbana nazo  katika jamii.

Halmashauri ya Mbozi kwa kushirikiana na shirika la savethechildren wameweza kuunda mabaraza ya watoto kuanzia ngazi ya kijiji, kata na hatimaye kufanikisha kuunda baraza la watoto ngazi ya wilaya ambalo lina washiriki kutoka kila kata 29, hali inayopelekea halmashauri ya Mbozi kuwa ya kwanza kufanya hivi kwa Mkoa wa Songwe.

Matangazo

  • No records found
  • Ona vyote

Habari Mpya

  • BARAZA LA WATOTO LAUNDWA MBOZI KUPIGANIA HAKI ZAO

    June 08, 2019
  • IGANYA NI KIJIJI CHENYE MAFANIKIO KUPITIA TASAF

    March 22, 2019
  • Ona vyote

Video

video zaidi

Kurasa za Karibu

  • You Tube
  • Katiba

Tovuti Muhimu

  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Ikulu
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

Watembeleaji wa kimataifa

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

writingMasterThesis

Eneo la ramani

Wasiliana nasi

    Mbozi

    Anuani: 3

    Simu: 025-2580272

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@mbozidc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hati Miliki 2017 Halmashauri ya Wilaya-Mbozi. Haki zote zimehifadhiwa